Friday, June 18, 2010

**Nchi ya Kitu Kidogo by Eric Wainaina**


Mzee alisema hakuna cha bure
Huo msema tumeutafsiri kinyume
Hata shule kuiingiza mtoto
Lazima utoe mchoto
Kupata simu ni balaa
Road license bei nafuu utanunua
Kupoteza ID ni mashaka
Twaarudisha Jamhuri yetu nyuma

Nchi ya kitu kidogolyrics from museke.com
ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe ndugu nenda Limuru


Hata nyumbani ukipatwa na majambazi
Kupiga 999 wasema, 'Sisi hatuna gari
Lete elfu tano ya petroli, saidia utumishi'
Mahakamani hela ndio haki
Kwa elfu chache mshtakiwa ndiwe mshtaki
Ushahidi hwa utajiri
Twarudisha Jamhuri yetu nyuma jamani

Nchi ya kitu kidogo
ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka soda ewe Inspekta burudika na Fanta
Nchi ya kitu kidogo
ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe Mama nunua Ketepa

Huko Kenyatta madawa zimeisha
Mashiti zauzwa marikiti mia kwa mia
Wafanyi kazi waenda miezi bil pesa
Ni bahati ukitibiwa
Mzigo wetu nazidi kuwa mzito
Watoto wanne na mshahara wa elfu mbili mia tano
Ya viatu, ya vitabu na vyakula
Nauliza na Mbotela
'Je, huu ni ungwana?'

Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe ndugu nenda Limuru
  • Stumble This
  • Fav This With Technorati
  • Add To Del.icio.us
  • Digg This
  • Add To Facebook
  • Add To Yahoo
blog comments powered by Disqus
 
Copyright 2010 Siteiya | Powered by Infoken Solutions.
Siteiya Sunshyn